Yatapita Lyrics
Nageuka kushoto naona watu wanalia
Natizama watoto wengi wanaangamia
Wengine wanadai eti huu ndio mwisho wa dunia
Ila Mungu pekee ndo anajua
Labda huenda maovu ndo yamezidi
Tunakoseea
Hivi watoto lini shule watarudi
Mtaani wanapotea
Wengine wanakosa mpaka hela ya kodi
Wanatolewa
Wasomi wa vyuoni nao lini watarudi
Tunawategemea
Binadamu tumezoea kuishi kwa upendo
Sasa imekuwa ni ngumu hata kupeana mikono
Kutembea kwa kujiamini hatuna uhuru tena
Ila ni changamoto wenda ndo tunapewa somo
Ila huenda yatakwisha
Yatapita
Ila huenda yatakwisha
Yatapita
Kukusanyika kufanya ibada
Nayo pia ishakuwa shida
Biashara nyingi zinakufa
Zinafungiwaa!!!
Vitu navyo bei vinapanda
Masikini tunasalenda
Hakuna dili hakuna tenda
Tunazidiwaa!!!
Ubaguzi wa rangi
Nao sasa washamiri
Weusi kuwekewa vigingi
Kufanyiwa ukatili
Michezoni lini itarudi tena
Matamasha yatarudi tena
Lini ndani tutatoka tena
Tuwe kama zamaninii
Binadamu tumezoea kuishi kwa upendo
Sasa imekuwa ni ngumu hata kupeana mikono
Kutembea kwa kujiamini hatuna uhuru tena
Ila ni changamoto wenda ndo tunapewa somo
Ila huenda yatakwisha
Yatapita
Ila huenda yatakwisha
Yatapita
Hii hali sasa, Itafika mwisho
Yatakwisha, yatapita
Ila huenda yatakwisha
Yatapita
(Ngatale Music)
No comments yet