Janga la Corona Lyrics

Ugonjwa huu kwa jina la Corona
Ulilipuka mwaka jana
Wuhan nchini China

Viongozi pamoja na wananchi
Sote tulidhani ni homa ya kawaida
Wanasayansi wakiwa na watafiti
Waliamua angalau kuisaka tiba yake

Kilicho tushangaza na kutuacha vinywa wazi
Ni kuwa Corona haina tiba
Wele huu ulizidi kuenea
Mpaka utakatangazwa kama janga la ulimwengu

Haukuenea Uchina peke yake
Bali hata mataifa mengine yaliadhirika
Vifo navyo vilianza kushuhudiwa
Hivyo basi watu wote tukashikwa na kiwewe

Madaktari walijaribu wawezavyo
Lakini juhudi zao hazikuweza kufua dafu

Hivi majuzi wakenya tulihuzunika
Kwa kusikia ati Corona hatimaye imewadia
Rais wetu Uhuru wa Kenyatta
Naye akatupasha kuwa janga limefika

Alitupa nazo njia za kujikinga
Na kuwasihi wakenya wote wazitilie maanani
Mambo mengi yalisitishwa humu nchini
Na pia safari zote za ndege zikakatizwa

Kumi na tano nao mwezi ni wa Marchi
Itakuwa kumbukumbu miongoni mwa wanafunzi
Shule zote ikiwemo za msingi
Za upili na hata vyuo navyo havikutengwa

Wanafunzi na haswa watahiniwa
Walirudi manyumbani ingawa shingo upande
Lililobaki ni kumsihi mwenyezi Mungu
Atuhurumie angalau atuondolee janga hili

Uwooiii, uwoooiii
Mola twakuomba tuepushe na janga hili
Uwooiii, uwoooiii
Mola twakuomba tuepushe na janga hili


Related Lyrics

Added by

Zikitu

SHARE

VIDEO

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Artists