Sawa Remix Lyrics
Amebadili tabia hayuko kama mwanzo
Usiku kucha kulia kaniacha na mawazo
Hajui mwenzake naumia kwa penzi la vikwazo
Na siku nikitulia natulia kunako
Sawa yote sawa
Itakuwa sawa kama tukiwa sawa
Hawa nimepagawa
Na penzi lako kama kuvuta madawa
Nikila tunda lako nahisi nina mabawa
Nikiona adui zako nawaonyesha powers
Taabani mahututi sijiwezi niko hoi
Penzi lako limenikwama kwenye koo sikohoi
Niko ndani stoki nnje hii vita sitoboi
Kuna giza nene ndani wapi koroboi?
Msamaha nautaka, msamaha nimekosea
Kuna njia nilikata nahisi kama nimepotea
Sawa, sawaaa
Sawa, sawaaa
Basi sawa nishakubali matokeo
Nenda tu salama japo nishakuzoea
Japo kisa mi sijui mpaka leo
Mpaka we unaondoka ni nini nilichokukosea?
Na bado nakuombea ili usije kupotea
Ulichokosa hapo ukipate unakoelekea
Mi nitakuwa sawa wa kwangu atatokea
Yea nitakuwa bie na maisha yataendelea
Nisipokubali kushindwa nitaanza kukonda
Nisipokubali kushindwa nitaenda kuroga
Nisipokubali kushindwa nitaanza kufosi
Alafu mapenzi ya kufosi ni kupotezeana muda
Okey sawa basi nenda
Inshallah Mungu akipenda
Tunaweza kurudiana tena ila sasa ooh no
No ushanitenda umeniachia kidogo sasa nahema
Sawa, sawaaa
Sawa, sawaaa
Si– mimi nakonda mimi
Nimekosa nisamehe nakiri kosa mimi
Ninachowaza wewe itakuwaje bila mimi
Nitaficha wapi sura yangu kelele za mjini (Sawaaa)
We huskiza propaganda
Za wasiotupenda ndo ukaamua kwenda (Sawaaa)
Unajua vile nilikupenda
Kwako nilisurender na leo we umeenda
Nakusaka kona zote my beiby sikuoni
Nateseka we uko wapi mah rudi nyumbani
Maruerue nikilala wanijia ndotoni
Najihisi ka peponi kuna muda motoni
Mama mia, nakuzimia
Wapi uliko mama kilio sikia
Kosa nilikosa haitojirudia
My dear mwenzio naumia yeah
Napata taabu nikikuona picha inanikera
Ile tulopigaga kabla ya kuzagaa
Aaah aah, nashika adabu huku majirani waninichora
Sa nitafanyaje mi si ndo nimekosea, sawa
Sawa, sawaaa
Sawa, sawaaa
No comments yet