Pitson

Nisaidie

Nisaidie Lyrics

Pitson -Nisaidie

Nisaidie Baba nisiwahi lala njaa
Nisaidie Baba nisipatwe na balaa
Hasara iwe mbali nami hata kwa biashara
Ninachouza wanunue nisibaki na bidhaa

Nisiwai kosa pesa ya kulipa nyumba ya kukodisha,
Pia unipe yangu nisiishi sana ya kukodisha
Jinsi ya kupata doo wewe Baba ndio utanionyesha,
Utatoa vitu vinavyonikondesha,
Aah aaah Nisaidie,
Aaah aaah Nisaidie,

Itakuwaje baba jirani ,
wanajua nimeokoka,
Na vile mimi ninateseka niko na deni hata kwa mama mboga,
Wamenidharau watakudharau,

Mungu wa Ibrahimu waonyeshe kwamba hujanisahau
Uh uh uh
Kama Shadrack Meshack Abedinego
Hata wanirushe kwenye moto
Nikikosa ya dunia bado sitawainamia

Sitawainamia
Ah ah Nisaidie
Ah Nisaidie
Ah ah Nisaidie
Ah Nisaidie

Kwa kila kitu nifanyacho Baba nisaidie, nisaidie
Kwa kazi ya mikono yangu Baba nisaidie, nisaidie
Uniweke mbali na balaa baba nisaidie, nisaidie


Related Lyrics

Added by

SHARE

VIDEO

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Artists