Maumivu ya Jaribu Lyrics
Japo jaribu limeruhusiwa na wewe Mungu
Hili jaribu linaumiza moyo
Japo jaribu limeruhusiwa na wewe mwenyewe
Hili jaribu linaumiza moyo
Japo maumivu haya Yesu wayajua haya
Moyo wangu unateseka
Japo haya yote wewe pekee wajua
Lakini moyo wangu unateseka
Nitie nguvu Baba yangu
Nitie nguvu Baba yangu
Naishi katikati ya watu
Wasiojua ni nini napitia
Natembea katikati ya watu
Wasiojua maumivu yangu
Kwa sababu ya mateso niliyo nayo
Nimejaribu kuelezea wengi
Pamoja na kuwaeleza ha
Bado hawajaelewa ninavyoteseka
Nilijua kwa kuwaeleza kwangu
Watajua nitesekavyo, hawakujua
Japo maumivu haya wewe Yesu wajua haya
Lakini moyo wangu unateseka
Eti naomba kwa unyenyekevu mkubwa
Usiniache jaribu likanimeza
Baba yangu mimi nimekubali kupita
Lakini usiniache
Nimekubali kupitia haya
Usiniwache nikamezwa na jaribu
Japo Ibrahimu aliitwa Baba wa imani
Moyo wake uliteseka
Japo Ibrahimu ulisema naye
Ukamwambia utampa watoto bado alilia
Pamoja na kwamba ulisema naye mwenyewe
Alipochelewa Isaka, Ibrahimu kalia
Japo alijua ni wewe Baba utampatia
Ibrahimu moyo uliuma
Kwa sababu Ibrahimu alichelewa kupata mtoto
Moyo wake uliteseka
Japo alijua Isaka ni mtoto wa pekee
Kwa sababu alichelewa alilia
Alijua utampa watoto wazuri
Lakini moyo wa Ibrahimu ulilia
Pamoja na kwamba unatufundisha
Majaribu lazma lakini mioyo inauma
Usituache Yesu, usituache wanao
Usituache wanao tukapotea
Usituache Baba, usituache oo
Usituache wanao tukaangamia
Usituache Yesu, usituache Baba
Usituache wanao tukapotea
Usituache Yesu, usituache Baba
Usituache wanao tukapotea
Usituache Yesu, usituache Baba
Usituache wanao tukapotea
Usituache Yesu, usituache Baba
Usituache wanao tukapotea
No comments yet