Maneno Lyrics

Lynn-Maneno

Nimezaliwa vuguruni
Miaka kadhaa imepita
Maisha ,ya hali duni
Nikahisi kuvunjika moyo

Kusota barabarani
Baba na mama malapa
Kuchekwa na majirani
Nusura ,nivunjike moyo

Mungu si adhumani
Akanipandisha cheo
Nikaitwa na Rayvanny
Tukashoot na video

Kiutani utani
Ukawa ndo ufunguo
Mara nikadate na fulani mmmh

Matusi kutukanwa
Na visa vyote visanga navumilia
Mengine yananichoma
Hadi yanafanya mwenzenu najililia

Mi bado mdogo sana
Mengine nashindwa kuvumilia
Kipi nimefanya kibaya
Mpaka mwenzenu nang’ang’aniwa

Aaah maana ni mengi kutwa kucha nasikia
Ati kuimba siwezi sawa nishazoea
Aaah maana ni mengi kutwa kucha wanaongea
Yatakauka machozi nami nitatulia

Sababu gani we rehani
Nipoteze nilichokitafuta
Kwa nia gani ya dhamani
Fadhila haishindwi kukumbuka

Niwaambie mimi sipati mimi
Kuwepo hapa nilipo,
Niombee yaaani mzazi wangu
Kokote huko mliko

Wote wametangulia,
Walonileta kwa dunia
Nimebaki peke yangu angalia,

Dua njema ,sasa ninawaombea
Mengi nakumbuka ninalia
Mpaka maumivu yananizidia

Matusi kutukanwa ,
Na visa vyote visanga navumilia
Mengine yananichoma
Hadi yanafanya mwenzenu najililia

Mi bado mdogo sana
Mengine nashindwa kuvumilia
Kipi nimefanya kibaya
Mpaka mwenzenu nang’ang’aniwa

Aaah maana ni mengi kutwa kucha nasikia
Ati kuimba siwezi sawa nishazoea
Aaah maana ni mengi kutwa kucha wanaongea
Yatakauka machozi nami nitatulia


Related Lyrics

Added by

SHARE

VIDEO

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Artists