LavaLava

Najidai

Najidai Lyrics

LavaLava-Najidai

Nenda mwambie aliniacha hohehahe
Zimfikie salama
Sasa nala pension, kochi kochi hodha ee
Nishapata kinyama tamu

Wala tusingefika mbali, niliona dalili
Bora kila mtu kivyake
Wala mapenzi si ujabari askari
Akadhani yuko peke yake

Sasa niko huru sitaki kusuffer
Nanenepa nina nuru bila maafa
Wale mandege makunguru walinichachafya
Mambo yakawa vururu kama taraafa

Sasa, najidai, najidai
Nimempata mpenzi
Oh sasa, najidai, najidai
Nimepata mtetezi

Mi sina wasiwasi
Nanenepea na zawauma roho
Oh sina mahaba ya mwendo kasi
Si twapeana wachafukwe ooh

Mi sina wasiwasi
Nanenepea na zawauma roho
Mwenzenu, sina mahaba ya mwendo kasi
Si twapeana wachafukwe ooh

Naweka wazi bila kwikwi
Hadharani nanena mnisikie
Mbona mtachonga viazi
Wanafiki mkikesha kusema ya kwetu sie

Mimi na yeye mpaka parapanda
Neng’enekeni
Karaukeni mshinde kwa waganga
Nazi vunjeni

Kaza neli endeleeni kuchamba
Yote semeni, semeni ila mtaisoma namba

Sasa niko huru sitaki kusuffer
Nanenepa nina nuru bila maafa
Wale mandege makunguru walinichachafya
Mambo yakawa vururu kama taraafa

Sasa, najidai, najidai
Nimempata mpenzi
Oh sasa, najidai, najidai
Nimepata mtetezi

Mi sina wasiwasi
Nanenepea na zawauma roho
Oh sina mahaba ya mwendo kasi
Si twapeana wachafukwe ooh

Mi sina wasiwasi
Nanenepea na zawauma roho
Mwenzenu, sina mahaba ya mwendo kasi
Si twapeana wachafukwe ooh, ooh

Hee mwenyewe twajinafasi
Hatutaki ushambena, hatutaki ushambena
Twakimwaya mwaya
Hatutaki ushambena, hatutaki ushambena

Mkomeni wenye roho mbaya
Hatutaki ushambena, hatutaki ushambena
Mahasidi wanaisaya
Hatutaki ushambena, hatutaki ushambena


Related Lyrics

Added by

Zikitu

SHARE

VIDEO

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Artists