Killy – Vumilia Lyrics

Mama nashindwa pata jibu kila swali ikiuliza
Mbona unanipa majaribu mpaka mbele naona kiza
Kweli nimekua eh, ambo wacha nijione
Mwili utadhoofu utapungua
Ona unataka nione
Unafungana virago vyote uliache pendo langu
Sifai eti, unatangaza kote
Hata kitanda sio cha kwangu
Kila siku unalia wee
Sijui ni kitu gani
Nakesha usiku kukusalia
Ila bado hunidhamini
Shida vumilia we
Wengine wanatamani
Usidanganyike usidanganyike
Ukajaniacha hasilani

Salima wa mama Mola nifanye wepesi
Mwenzako kwa kina nishazama moyo unadunda kitenesi
Salima wa mama Mola nifanye wepesi
Mwenzako kwa kina nishazama moyo unadunda kitenesi
Nakuomba vumilia, vumilia, vumi vumi vumilia
Ata tukishindia karanga, vumi vumi vumilia
Najitafuta ndo najichanga mama, vumi vumi vumilia
Oh we ndo kichuna cha moyo wangu vumi vumi vumilia
Siri yako siri yangu
Lololo, lolololo, lolololo, lololo

Ah umenikamata usizime taa nitakuwa kizani oh (Gizani)
Mbona kidogo nikipata nalete mkono uende kinywani oh (Kinywani)
Mama utanivuruga ubongo, utanizika nitarudi kwa udongo
We ndo kipendacho roho mi kilema siwezi tembea bila magongo
Kila siku unalia wee
Sijui ni kitu gani
Nakesha usiku kukusalia
Ila bado hunidhamini
Shida vumilia we
Wengine wanatamani
Usidanganyike usidanganyike
Ukajaniacha hasilani

Salima wa mama Mola nifanye wepesi
Mwenzako kwa kina nishazama moyo unadunda kitenesi
Salima wa mama Mola nifanye wepesi
Mwenzako kwa kina nishazama moyo unadunda kitenesi
Nakuomba vumilia, vumilia, vumi vumi vumilia
Ata tukishindia karanga, vumi vumi vumilia
Najitafuta ndo najichanga mama, vumi vumi vumilia
Oh we ndo kichuna cha moyo wangu vumi vumi vumilia
Siri yako siri yangu

Related Lyrics

Added by

Zikitu

SHARE

VIDEO

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Artists