Ibraah – Maumivu Lyrics

Mungu ndo aliumba mbalamwezi na jua
Na tena kwa majira tofauti kutustiri
Ah ona ye pekee ndo anayetambua
Yupi anasema ukweli na yupi msiri
Ah na asikwambie eti kwamba niko
Sawa usisikie uwe ndo pacha kwa mbali unanikwaza
Basi nihurumie marafiki wasifanye unichukie
Moyo kukataza kwa mbali nawe najikaza, siyawezi
Huwenda nasubiria ndoto ambayo haiwezi timia ila ni sawa
Nitajua tu ni changamoto kweli umedhamiria mabaya
Mbona nilikupa moyo utunze we unaugawa
Unachoniachia ni maumivu kwenye upendo wetu

(unachonipa ya kwamba)

(Umeniacha na nani) sasa ni nani wa kunisitiri unafikiri
(Umeniacha na nani) nimekuwa dhaifu inauma na roho
(Umeniacha na nani) hata huruma hauna ah hauna aaah
(Umenicha na nani) nani ihi, ni nani umeniacha na yeye

Sitaki kuwa kobe la mchana kipitacho mbele
Nikakobelea tu na hisia siwezi zidanganya
Nimezama nishakuzoea boo
Mapigo ya moyo yatafeli kweli
Isigeuke vita karaba na kirikuu, tuliahidi si tutapendana
Tutasemaheana sa mbona unaniruka weee
Nawaza kwa mganga nikupige ndele
Moyo unaniambia niache kiherehere, maana ni hasara hasara
Na najipa imani we ndo wangu wa milele mi nimefall mjukuu wa Nyerere
Kifuano utalala, utalala ah
Huwenda nasubiria ndoto ambayo haiwezi timia ila ni sawa
Nitajua tu ni changamoto kweli umedhamiria mabaya
Mbona nilikupa moyo utunze we unaugawa
Unachoniachia ni maumivu kwenye upendo wetu

(unachonipa ya kwamba eeeh)

(Umeniacha na nani) sasa ni nani wa kunisitiri unafikiri
(Umeniacha na nani) nimekuwa dhaifu inauma na roho
(Umeniacha na nani) hata huruma hauna ah hauna aaah
(Umeniacha na nani) nani ihi, ni nani umeniacha na yeye

Mmh ah oye yeye ah, chinga ah
Konde Music Worldwide
Nawaza kwa mganga nikupige ndele
Moyo unaniambia niache kiherehere, maana ni hasara hasara
Na najipa imani we ndo wangu wa milele mi nimefall mjukuu wa Nyerere
Kifuano utalala, utalala ah

Related Lyrics

Added by

Zikitu

SHARE

VIDEO

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Artists