Simu Lyrics

Hallo Baba Ni Mimi Mwanao,
Hii Namba Nimechukua Yeremia Hapa,
Inasema niite,Nitakuitikia, Nitakuonesha Magumu Usiyoyajua Mwanangu,
Haya Leo Simu Yangu Hii,
Napiga Kwa Imani Tuu,
Nakuomba Sikiliza Dadii,
Naumia Moyoni,
Unaweza tunasuru na Hili na Hili,
Manabii wale Baba Ungewaambia Kuna Corona,
Au Tunadanganywa Ni Bandia Wanayoonaga,
Je Umekaa kimya Ukitazama wanayofanya,
Mbona mwaka Jana Walitwambia Huu Ni Mwaka Wa Bwana,
Tumekaa Mwaka Ulianza Shwari,
Asahivi Hatuelewi,
Kila Saa Alama Ya Hatari,
Ni mbaya Habari,
Wamekufa Saba, Walikufa Sita,
Mara ooh Mnadanganywa,
Wamefika Kumi,

Mmmh, Acha Nisanitaizi Oooh,
Barakoa Kidogo,Nisishike Pua
Mmmm na
Mmh Acha Nisanitaizi mmmh
Barakoa Kidogo Nisishike Macho
(Wakatai Nasubiri) Mmmh Mmh.

Heri Matajiri Tajiri, Wanaweza Kununua Maski,
Wengine Hizo Bei zake,
Ndo Tunategemea Tule,
Mama Mamaa, Muda Wote Ni Presha,
Maana Watoto wake Maisha Ndo Wanatafuta,
Kwa Siku Kupata Kwa Siku Tumezoea,
Hatuna Maisha Kabisa ya Akiba,
Usipotuhurumia Wewe ndo Tumekwisha,
Usipotuhurumia Wewe ndo Tumekwisha,
Niliongea na Waombaji Nikawaambia Tusiache Kuomba,
Maana Adui Ametu nia Mabaya, MMH
Mi Nakuamini kuamini, Kuamini Baba,
Mi Nakuamini, Nina Kuamini,

Mmmh, Acha Nisanitaizi Oooh,
Barakoa Kidogo,Nisishike Pua
Mmmm na
Mmh Acha Nisanitaizi mmmh
Barakoa Kidogo Nisishike Macho
(Wakatai Nasubiri) Mmmh Mmh
ACHA NI SANITAIZI


Related Lyrics

Added by

Zikitu

SHARE

VIDEO

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Artists