Hasara Roho Lyrics

Penda nipende nikiwa hai
Sio nikifa
Na tena ni bora uniambie
Ukiniona

Vile unavyonisaidia
Usinitangaze
Utanisitiri Bwana wewe

Usicheke (Usicheke)
Maana kesho huoni (Hauoni)
Ya duniani ni siri
Kupita za moyoni

Tena niombee
Nami niwe na heri
Kati ya wenye furaha
Sitakusumbua

Kama shilingi (Shilingi) Manoti (Manoti)
Yaani hizo ni per diem zisikuchanganye
Kesho firimbi (Firimbi) Kama roboti (Roboti)
Haya maisha ni gwaride yasikuchanganye

Hasara roho, hasara roho
Hasa basi basi tukumbukane
Hasara roho, hasara roho
Hasa basi basi tukumbukane

Washatabasamu walau kwa moja
Ipaki kwenye moyo usipandishe vioo
Maisha ni tofauti ukishiba shukuru
Ona walio wengi wanalia na njaa

Na kama huwezi nisaidia
Usiniumize
Ya duniani ni siri
Kupita za moyoni

Tena niombee
Nami niwe na heri
Kati ya wenye furaha
Sitakusumbua

Kama shilingi (Shilingi) Manoti (Manoti)
Yaani hizo ni per diem zisikuchanganye
Kesho firimbi (Firimbi) Kama roboti (Roboti)
Haya maisha ni gwaride yasikuchanganye

Hasara roho, hasara roho
Hasa basi basi tukumbukane
Hasara roho, hasara roho
Hasa basi basi tukumbukane


Related Lyrics

Added by

Zikitu

SHARE

VIDEO

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Artists