Unibebe Lyrics
Natamani unikumbuke
Japo kwa salamu tu
Moyo wangu ufarijike
Nami nipate nafuu
Usitake nisumbuke
Nihangaike ka kikuu
Machozi yanibubujike
Kama nakata vitunguu
Upendo wangu kwako cheche
Yani nisumbuke unifikirie
Nimelowa tepe tepe
Simama kidete, unishikilie
Majirani wanasema mengi
Kisa nini, eti wewe hunipendi
Shukurani ya punda ni mateke
Kukuweka ndani hayo ndo malipo yake
Eeh Baba, nami nahitaji unibebe
Eeh Baba, nami nahitaji unibebe
Eeh Baba, nami nahitaji unibebe
Eeh Baba, nami nahitaji unibebe
Matatizo yananizonga, maadui wananisonga
Eh Baba, Baba Baba Baba
Hata ungenipa vidonda, mi singechoka kukuomba
Eh Baba, Baba Baba Baba
Ila bado sijachoka napambana
Kina ikibidi nakazana
Japo mengi yananichanganya
Ila bado sitokata tamaa
Sijachoka napambana
Kina ikibidi nakazana
Japo mengi yananichanganya
Ila bado sitokata tamaa
Eeh Baba, nami nahitaji unibebe
Eeh Baba, nami nahitaji unibebe
Eeh Baba, nami nahitaji unibebe
Eeh Baba, nami nahitaji unibebe
Ukiniacha nasononeka aha
Gizani natetemeka
Ukiniacha nasononeka ah ah
Nakuhitaji
Ukiniacha nasononeka
Gizani natetemeka
Nakuhitaji
No comments yet