Ongeza Lyrics
Diamond Platnumz – Ongeza Lyrics
Mi kwako sikuingia Miguu
Mikono Hadi Kichwa Kiufupi Mazima
Nikiamini Wakufa kuzikana
Yani moyo si Nafuu Nahututi hata mashaka sina
Nikiamini nitatengwa na Maulana
Mvumilivu hula mbivu nimengoja mpaka zikaoza
Naambulia maumivu ningali sina wa kunipoza
Sijui yangu stahimilivu kunyenyekea waniponza
Napambania utulivu mwezangu chuki unaikoza
Sikukufuta tu machozi ulipolia nililia na wewe
Sasa mbona wanilipa majonzi yaani stress mapombe mi nilewe
We ndo wangu Yesu Mkombozi sa mbona Petro unaniacha mwenyewe
Nikose usingizi na njozi ndo ufurahi okay sawa
Si unataka nitukanwe Ongeza ongeza bado
Nidhalilike Ongeza ongeza bado
Nikose pa kuificha sura Ongeza ongeza bado
Marafiki wanicheke, waning’onge ada Ongeza ongeza bado
Kisichokuua hukukomaza
Ati ikiwa sikani huo msemo nakataa
Maana jua linapoangaza na sina afadhali mi kwangu ni mabalaa
Oh najitahidi kumsinga mwali Ila somo ananikataa
Oh penzi letu si la kibatari Anayamwaga mafuta taa
Kutwa ni vurugu ndani purukushani hapakaliki
Roho inaniuma yaani kwanini sa tunagombana sweetie
Oooh njema gani niambie labda nitende kipi
Hata pa kucheka hunnie Ati utani unapanic
Naelewa riziki mafungu saba na la kwangu sita
Naelewa sikutoshi labda kukuridhisha
Sikukufuta tu machozi ulipolia nililia na wewe
Sasa mbona wanilipa majonzi yaani stress mapombe mi nilewe
We ndo wangu Yesu Mkombozi sa mbona
Petro unaniacha mwenyewe
Nikose usingizi na njozi ndo ufurahi okay sawa
Si unataka nitukanwe ongeza ongeza bado
Nidhalilike ongeza ongeza bado
Nikose pa kuificha sura ongeza ongeza bado
Ndugu jamaa wanicheke, waning’onge ada ongeza ongeza bado
Haaa nikose pa kuificha sura
Waning’onge ada
No comments yet