Binadamu Lyrics
Christian Bella-Binadamu
Mama haya dunia
yana mambo mengi
Utakuta unapenda
kuishi na binadamu
Lakini kila siku
wanakugeukia
Wakikukwepa kuna siku watakutafuta
Wakikusengenye nyamaza watajifunza
Wakikudharau ipo siku watakusifia
Ni kawaida yao, kawaida yao
Tenda wema nenda zako usingoje shukurani
Ona binadamu wabaya,
Ubinadamu ni kazi wabaya
Watu wa dunia wabaya,
Dunia sisi ni binadamu tunapita,
Dunia ya Mola, tenda mema
Unajiwekea akiba kwa Mungu Baba
Amini raia dunia itapita
Mungu akikujali usidharau wenzio
Ukipata kidogo saidia wasiojiweza
Tenda mema duniani usingoje shukurani
Kuna binadamu ni wa ajabu sana
Hawapendi kuona maendeleo ya wengine
Watakuchekea usoni
Ukiwapa kisogo wanakumaliza kabisa
Hawana maana
Watakufuata kama unacho
Ukikosa kabisa wanakumaliza kabisa
Ni binadamu
Mwenzako akipata usinune
Fanya na wewe ujitume
Chuki hawezi kuwa mfalme
Ndo maana lima kesho uvune
No comments yet