Balaa Mc

We nani

We nani Lyrics

Balaa Mc-We Nani

We nani, Hallo hallo
We nani,Hallo hallo(×2)

Dah, ina maana ulifuta,
Siri ya zimenisahau kabisa,
Sawa kitambo kidogo, miaka sasa imepita,
Ila sio kweli unisahau kabisa

Ila sawa, naskia umeolewa mwana,
Tena una mtoto umefanana nayeye sana
Hongera hongera mama
Mi bado nipo naendelea kupambana,

Mi ndo yule, ulonidanganya unanipenda
Kisa umasikini ,ukaniacha ukaenda
Ulitaka nyama ulishindwa, kula mrenda
Mwisho wa siku ukanitoroka ukaenda

Ila kipi ulitaka sijakupatia,
Mapenzi ya dhati ,nilikuonyeshea
Kuzingatia nilikuzingatia,
Kwa mama Sara kijona nilikulipia

Hatugombani ,nakukumbusha tu
Ishi kwa amani, usiishi roho juu
Simu yangu si ya, ugomvi nilikumiss tu
Japo umeondoka ila moyoni unaishi

Ila sawa, naskia umeolewa mwana
Tena una mtoto umefanana nayeye sana
Hongera hongera mama
Mi bado nipo naendelea kupambana

We nani, Hallo hallo
We nani, Hallo hallo(×2)

Jamani hii, hii, nikuogope
We eti nisibakie nikuogope wewe
Hii, hii, akuogope
We eti asicheze chura akuogope wewe

Shika chini we, dada usiangalie sura
Tikisa moja moja sijaona ukicheza chura,

Hii, hii, nikuogope
Haunilishi haunivishi nikuogope wewe
Hii, hii, nikuogope
Sikujui hunijui nikuogope wewe

Sina fagio fagio langu la chuma,
Kwanza hatuendani mi mzingua sijui mwenzangu,
Sina fagio fagio, langu la chuma
Kwanza hatuendani mi makonde sijui mwenzangu

Jamani umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu
Na mi ni mwanadamu isipokuwa nina mapungufu

Jamani we mcheza kususia
Na sijaona ukisusa
Hilo amekupa amekususia


Related Lyrics

Added by

Zikitu

SHARE

VIDEO

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Artists